1 Juni 2026 - 19:05
Ayatollah Amoli Larijani: Wananchi wa Iran Wanasimama Pamoja na Lebanon

Mwenyekiti wa Baraza la Utambuzi wa Maslahi ya Mfumo wa Iran, Ayatullah Sadeq Amoli Larijani, amesema wananchi wa Iran wanaendelea kusimama pamoja na Lebanon, akieleza kuwa ni wajibu wa kihistoria na wa kiutu kuunga mkono taifa hilo katika kukabiliana na mashambulizi ya Israel.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mwenyekiti wa Baraza la Utambuzi wa Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sadeq Amoli Larijani, amesema kuwa wananchi wa Iran wanasimama bega kwa bega na wananchi wa Lebanon katika safu ya Muqawama (Mapambano ya Upinzani), huku akisisitiza mshikamano wa kihistoria uliopo kati ya pande hizo mbili.

Katika ujumbe aliouchapisha kupitia mitandao ya kijamii kwa lugha ya Kifarsi na Kiarabu kufuatia ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, Ayatullah Amoli Larijani alisema kuwa wananchi wa Iran wana wajibu wa kusimama pamoja na taifa la Lebanon ambalo limechagua njia ya kusimama imara na kujitolea kwa ajili ya heshima na uhuru wake.

Alieleza kuwa Hizbullah ya Lebanon ni alama ya muqawama wa wananchi ambao katika nyakati ngumu zaidi ilisimama kwa mshikamano pamoja na wananchi wa Iran, na kwamba kwa uaminifu na kujitolea kwake imeacha alama kubwa katika historia ya eneo hilo.

Ayatollah Amoli Larijani aliongeza kuwa katika kipindi hiki ambapo Lebanon inakabiliwa na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni, wananchi wa Iran wanaendelea kusimama pamoja na wananchi wa Lebanon katika safu ya muqawama ili kutimiza wajibu wao wa kiutu na wa kihistoria kwa taifa ambalo limeonyesha uthabiti mkubwa licha ya changamoto zinazolikabili.

Kauli hiyo imekuja wakati mashambulizi dhidi ya Lebanon yanaendelea kuzua hisia na mwitikio kutoka kwa viongozi na taasisi mbalimbali katika eneo la Mashariki ya Kati.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha